Wapiga
kura wanaelekea kwenye vituo vya kupigia kura nchini Musumbiji leo
kumchagua rais mpya na wabunge kwenye uchaguzi wenye upinzani mkali
tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1975.Chama tawala, cha Frelimo, ambacho kimekuwa mamlakani tangu mwaka 1975, kinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa chama cha upinzani cha Renamo.
Mgombea wa chama tawala ni Filipe Nyusi, ambaye ni waziri wa zamani wa ulinzi.Msumbijini moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi barani Afrika na mshindi wa uchaguzi atahakikisha rasilimali za nchi ikiwemo gesi zinatumiwa vyema.