Miss Tanzania 2014/15 Sitti
Ushindi wa Sitti umezua mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na mashabiki waliohudhuria mashindano hayo kuonyesha wazi wasiwasi wao kuwa mrembo huyo ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu hakustahili kushinda kwani alitoka nje ya mstari katika kujibu swali linalohusu uzazi wa mpango.

Katika kujibu swali hilo ambalo lilikuwa la
kuchagua lugha kati ya Kiswahili na Kingereza, Sitti alichagua
Kingereza, lakini aliwaacha watu midomo wazi kwani alitumia lugha ya
Kifaransa.
Kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Sitti alikuwa na
mashabiki wengi ambao walitoka Temeke wakiwa na mabango ya kumnadi kuwa
ndiye Miss Tanzania.
“Katika majaji ni nani anayejua lugha ya Kifaransa
alichokijibu wanakielewa, tulijua tangu mwanzo yeye ndiye atapewa,
maana hata kwenye Televisheni za ukumbini anaitwa mwingine picha
inayoonyeshwa ya kwake,” alisikika mmoja wa mashabiki baada ya Sitti
kutangazwa mshindi.
Hata hivyo, Mratibu wa mashindano hayo, Hashimu
Lundenga alisema, “Wasichana wengi ni wazuri, kila mmoja alistahili
kushinda na maneno kama hayo ya upendeleo tumeshayazoea hakuna mwaka
ambao mshindi katangazwa yakakosekana maneno.”
Katika mashindano hayo mshindi wa pili alikuwa
Lilian Kamazima, wa tatu ni Jihan Dimachk, nafasi ya nne ilienda kwa
Dorrice Mollel huku Nasreen Abdul akichukua nafasi ya tano.
Taji la Photogenic lilinyakuliwa na Evelyne Baasa,
vipaji maalumu lilienda kwa Nicole Sarakikya, taji la Personality
limetwaliwa na Salama Salim, huku lile la Top Model likichukuliwa na
Jihan Dimachk.