Tuesday, September 9, 2014

AZAM FC YAIWINDA YANGA NGAO YA HISANI JUMAPILI

KOCHA wa Azam, Joseph Omog, amesema washambuliaji wake wanne anaowachezesha kwa pamoja klabuni hapo wamepewa jukumu la kufunga ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.

Omog hutumia mfumo wa 4-2-4 kwa kuwachezesha John Bocco, Leonel Saint Preux, Kipre Tchetche na Hamis Mcha kwa wakati mmoja. Azam inaendelea na maandalizi yake ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaochezwa Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Omog alisema kati ya mastaa wote wanne hakuna aliyepewa jukumu la kipekee kwani wote wanatakiwa kufunga wanapopata nafasi lakini amesisitiza washambulaji hao kuendelea kucheza kwa ushirikiano.


“Kila mtu anatakiwa kufunga, hiyo ndiyo dhamira ya kuwachezesha wote kwa pamoja, hakuna niliyempa jukumu kubwa zaidi ya mwingine, la muhimu hapo ni kutengeneza nafasi na kufunga,” alisema.

“Kikubwa hapa ni kwamba nataka timu iweze kucheza kwa ushirikiano, washambuliaji wakipoteza mpira wanatakiwa kurudi kwenda kukaba na wakipata mpira wanatakiwa kupanda kwa pamoja kwenda kufunga. Kazi hii itaanzania kwa Yanga.