Monday, September 8, 2014

MTITIGAME AELEZEA KILICHOMUONDOA BONGOMOVIE

KATIBU Bongo Movie Unity William J. Mtitu ‘Mtitu’ amemwaga manyanga baada ya kundi hilo kukumbwa na kashfa ya ulaji wa michango ya fedha katika matukio mbalimbali.

Mtitu alisema kwa heshima yake na kampuni yake amejiuzulu ili kukwepa fedheha.

“Kuna mambo mengi ambayo yanafanyika katika kundi hili ambayo hayafuati utaratibu, nimejitahidi sana kujaribu kuyaweka sawa kwa mustakabali wa tasnia ya filamu lakini wenzangu hawanielewi,” alisema.


“Sasa kwa heshima yangu na kampuni yangu nimekwepa fedheha, bora nifanye kazi zangu kuliko kutumikia fikra za mtu, nimejizulu sitaki kushiriki upuuzi,” anasema Mtitu.

Mtitu anasema kuwa mwenyekiti wake amekuwa akijiamulia na kuandaa vitu bila majadiliano na uongozi wa Bongo Movie Unity. Hivi karibuni kundi hili limechafuka kwa tetesi zinazosema kuwa limegeuza mtaji wa kujinufaisha kwa matukio ya misiba na matamasha na pesa hizo zikiwafaidisha baadhi ya viongozi tu na si kikundi.