Dokii ni rafiki mkubwa wa Lucy Komba na mwenyewe amesema wametoka mbali hivyo aliamua kumzawadia kiwanja kilichopo Bagamoyo kama kumbukumbu ya urafiki wao.
Akizungumza hivi karibuni Dokii aliyetoa performances nzuri katika filamu za Mdundiko na Kisate alisema "Mimi na Lucy tumetoka mbali, tumeshirikiana katika mengi na kudhihirisha upendo wangu kwake namzawadia kiwanja cha eka moja kilichopo Bagamoyo, naamini itakuwa ni kumbukumbu nzuri ya urafiki wetu"
Harusi ya Lucy Komba na mchumba wake mzungu raia wa Denmark inatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, Jijini Dar es salaam na sherehe nyingine kufanyika Denmark.
Lucy Komba katika Kitchen Party yake
