Friday, September 5, 2014

Ubelgiji yaichakaza Australia

Dries Mertens

Ubelgiji waliofuzu robo fainali ya Kombe la Dunia, waliendeleza umaahiri wao kwa kukomesha Australia 2-0 Alhamisi kwenye mechi ya kujipima nguvu.

Mabao katika kila kipindi kutoka Dries Mertens na Axel Witsel yaliongoza vijana wa Marc Wilmots kuzoa ushindi utakao watia joto kabla ya kuanza kampeni yao ya kufuzu kombe la Ulaya la 2016.

Straika wa Napoli Mertens alifungua udhia dakika ya 18 kabla ya Witsel anayechezea Zenit St. Petersburg kuongezea la pili na mkwaju rojo rojo ikisalia chini ya robo saa mechi kukatika.


Kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama, mechi yao dhidi ya Israeli kwenye kampeni ya kufuzu Kombe la Ulaya iliyopangiwa Jumanne ijayo imesukumwa hadi Machi 31 mwakani.