|
|
Meneja wa Uingereza Roy Hodgson, alipandwa na
gadhabu na kurusha cheche za matusi kwa wanahabari waliotaka majibu ya
sababu za mchezo wao duni katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Norway
Jumatano.
Nahodha mpya, Wayne Rooney, alifunga penalty katika kipindi cha pili kuamua mechi hiyo lakini hiyo ndio ilikuwa nafasi ya pili pekee kulenga goli la wapinzani wao katika kipindi chote cha mechi hiyo.
Mashabiki 40,181 walitizama mechi hiyo, idadi ndogo zaidi kuwahi shuhudia mechi ya Uingereza katika uga mpya wa Wembley huku England wakitoa jasho kwenye emchi yao ya kwanza tangu kufedheheshwa katika Kombe la Dunia.
Alipoulizwa kiini cha kuendelea kudorora kwa timu hiyo, Hodgson alipandwa na hasira na kukemea wanahabari.
“Kabla ya Kombe la Dunia, tulivutia mashabiki 75,000, 80,000 kutizama tukicheza na Peru ambao kwa ukweli, si wapinzani wagumu kama hawa wa leo (Jumatano).
“Sasa tuna 40,000 kuona tukicheza dhidi ya wapinzani wakali zaidi na sina uwezo wa kurekebisha hali hiyo kwani siwezi kurudisha saa nyuma,” Hodgson alisema.
“Chenye naweza kufanya ni kuchunguza chenye nimeona leo na kutoa uamuzi kupitia macho yangu, sio kutoa uamuzi juu mtu ataniambia tulibuni nafasi mbili pekee. Hilo kwangu ni ******* ******. Samahani,” alifoka.