Tuesday, November 4, 2014

UNITED WANAKOSA UBORA- CARRICK

Michael Carrick

Nyota wa Manchester United, Michael Carrick, amekiri klabu hicho cha ligi ya Premier ya Uingereza kimekosa ubora unaohitajika kubobea kufikia sasa musimu huu lakini amepigia miamba hao upatu kuimarisha matokeo yao duni. 
 
Kufuatia kusalimu amri ugenini kwa maadui wao wa jadi, Machester City Jumapili, United wamezoa alama chache katika mechi 10 za kwanza za mwalimu wao mpya Louis Van Gaal kuliko zile walipata chini ya mtangulizi wake aliyefurushwa, David Moyes.

United wamejipata alama 13 nyuma ya vingozi Chelsea na alama sawa na pengo hilo lakini Carrick amesisitiza United wako kwenye mkondo wa kutamba tena hivi karibuni.

“Tukiangalia jumla ya alama zetu, tunajuta pakubwa kwani hatuko katika kiwango kinachohitajika. Lakini ukichunguza kwa makini, kuna dalili tutakuwa na musimu mwema.


“Kuna mambo machache ambayo yanatwendea kombo na tunajipata tukifanya makosa kidogo kidogo lakini kwa ujumla, hisia zimetanda kuwa tunajenga kikosi kitakacho fanikiwa,” mchezaji huyo alisema.