Tuesday, November 4, 2014

AZAM FC NAKO KWAWAKA MOTO.

Kufuatia kupata vipigo viwili mfululizo toka kwa JKT Ruvu ya Pwani 1-0 na Ndanda FC ya Mtwara 1-0 hali si shwari ndani ya klabu ya Azam FC baada ya kocha wake msaidizi Kalimangonga Ongalla kubwaga manyanga.

Taarifa za ndani toka Azam zinasema Ongalla ameamua kujiuzulu nafasi yake hiyo na ataondoka nchini kuelekea Uingereza kujiendeleza na taaluma yake ya ukocha.

Lakini mtandao huu umebaini kuwa vipigo viwili mfululizo ndio vimepelekea kocha huyo kubwaga manyanga.

Azam imekuwa na wakati mgumu ktk mechi zake za karibuni, mabingwa hao wa bara 2013/14 wamejikuta wakitibua rekodi yao ya kucheza mechi 38 bila kupoteza.

Azam inayonolewa na Mcameroon Joseph Omog imekubali vipigo toka kwa JKT Ruvu cha bao 1-0 ktk uwanja wake wa Chamazi, pia ikakubaki kipigo kingine cha ugenhni toka kwa Ndanda FC 1-0 ktk uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.


Ongalla ameamua kujiuzulu kutokana na mwenendo mbaya wa timu, huenda kocha mkuu naye akajiuzuru endapo itapoteza mchezo mwingine.