Monday, November 3, 2014

Villa wateleza na kulazwa na Spurs

Harry Kane

Aston Villa walifunga bao lao la kwanza baada ya kukaa zaidi ya saa tisa bila bao lakini mambo yakawaendea mrama Christian Benteke alipofukuzwa uwanjani na Tottenham Hotspur wakajikwamua na kushinda 2-1 mechi iliyochezewa Villa Park Jumapili.

Hilo kilikuwa kichapo cha sita mfululizo Ligi ya Premia, licha ya Andreas Weimann kumaliza ukame wa mabao kwa kufunga krosi ya Charles N'Zogbia dakika ya 16.

Lakini straika wa Ubelgiji Benteke alifukuzwa uwanjani dakika ya 20 baada ya kipindi cha pili kuanza kwa kumgonga Ryan Mason usoni kwa kutumia mkono wake baada ya mtafaruku uliohusisha wachezaji kadha.


Nacer Chadli alisawazisha kupitia kona dakika sita kabla ya mechi kumalizika muda mfupi kabla ya Harry Kane kufunga bao kupitia frikiki iliyogonga kichwa cha mchezaji wa Villa na kujitoma wavuni.
Ushindi huo uliwabeba Spurs hadi nafasi ya nane, na kuacha Villa nambari 15, alama mbili kutoka eneo la kushushwa daraja.