Msanii mwenye maskani yake Hale mkoani Tanga Mkola Man amewaambia mashabiki wake kuwa anakuja na ujio mpya hivi karibuni na wakae mkao wa kula, akizungumza na mtandao huu, amesema anatarajia kuja na nyimbo mbili mpya ambazo zote ni kali.
Msanii huyo ambaye anasifika kwa uwezo wake wa kutunga mashairi na kurap amesema anamalizia kazi yake ya mwisho studio na muda wowote itakuwa tayari,'Mashabiki wangu jiandaaeni kupokea ujio wangu mpya baada ya kimya kirefu', alisema Mkola Man ambaye jina lake halisi Christopher Mhenga.
Mkola Man liatamba na nyimbo zake kadhaa huko nyuma ambazo zilimfanya akubalike mpaka kuingia katika top ten za vituo mbalimbali vya redio hapa nchini, hivi karibuni msanii huyo amekuwa gumzo katikia mitandao ya kijamii kuhusishwa na dini ya freemason.
Hata hivyo mwenyewe amesema atalizungumzia kiundani lakini si mapema kusema sasa kwani kuna makubwa yamefischika juu ya hilo
