Monday, October 13, 2014

Meneja Supershine aja na wazo la kuunda chama cha waimba taarabu

Na Mwandishi wetu

Meneja wa kundi kongwe la muziki wa taarabu nchini la Supershine Modern Taarabu lenye maskani yake Magomeni jijini Dar es Salaam. Kaisi Mussa Kaisi amekuja na wazo jipya lenye kuleta tija kwenye tasnia ya muziki wa taarabu.

Akizungumza na Ubuyu wa Taarabu, Kaisi amesema kwa sasa anataka kuwashawishi wanamuziki wa taarabu pamoja na wadau kuanzisha chama chao kwa lengo la kuusaidia muziki huo kusonga mbele, Kaisi amedai muziki wa taarabu ndio muziki mkongwe kuliko wote nchini lakini anashangaa kuachwa nyuma kimaendeleo.

Taarabu ilianza tangia mwaka karne ya 13BK walipoingia Waajemi ambapo walipitia Zenji sasa Zanzibar, Kaisi anadai kushamili kwa muziki kumepelekea kusambaa pwani zote za Afrika mashariki na kati, lakini Tanzania inaonekana kupiga hatua katika muziki huo hasa baada ya kuanzishwa makundi mbalimbali.


Meneja huyo ambaye si muongeaji sana ila ni makini kwa vitendo amedai kuachwa nyuma kwa muziki huo kimaendeleo imetokana na baadhi ya wanamuziki na wadau kujisahau hivyo anawataka kuanzisha umoja wao ili uweze kuwasaidia kwa namna yoyote ile.

Kundi la Supershine limeanza kufanya vizuri tangia kumpata meneja huyo ambaye awali alikuwa katika kundi la T-Moto ambalo kwa sasa linasuasua, mawazo ya Kaisi yakitimia anakuwa Mtanzania wa kwanza kuwawezesha wanataarabu kupata chama chao kama ilivyo kwa muziki wa dansi nk